Ingwe yamaliza ya tatu Mozzartbet Cup baada ya kuibana Sharks

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya AFC Leopards imechukua nafasi ya tatu katika makala ya mwaka huu ya mashidnano ya kuwania kombe la Mozzzart, baada ya kuibwaga Kariobangi Sharks mabao 2-1 .

Mechi hiyo ya nafasi ya tatu na nne imesakatwa Jumamosi katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex.

Leopards almaarufu Ingwe walitawala kipindi cha kwanza wakitwaa uongozi kunako dakika ya 16 kupitia kwa mshambulizi Victor Omune, kabla ya beki  Bakari Randy kuongeza la pili katika dakika ya 33.

Sharks  walirejea kwa vishindo huku wakikomboa goli moja katika dakika ya 73 kupitia kwa Keith Imbali.

Leopards wametia kibindioni shilingi laki saba unusu kwa ushindi huo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *