Ndoto ya Ingwe kucheza soka ya Afrika yafyatuliwa na Police

Dismas Otuke
1 Min Read

Matumaini ya Klabu ya AFC Leopards kurejea katika soka ya bara Afrika msimu ujao  yameyeyuka baada, ya kushindwa bao 1-0  na Police FC katika nusu fainali ya kombe la Mozzartbet Jumatatu Adhuhuri.

Nusu fainali hiyo ilitibuka Jumapili kunako dakika ya 60  baada ya refa kujeruhiwa na mashabiki, wakati ambapo Police FC walikuwa wakiongoza goli 1 kwa bila.

Nusu fainali hiyo ilisakatwa katika kiwara cha Police Sacco mtaani South C.

Ingwe mashindano ya Afrika kwa mara ya mwisho mwaka 2010 walipobanduliwa katika awamu ya mchujo ya kombe la shirikisho.

Police sasa watakabiliana  na Kenya Commercial Bank kwenye fainali ya Juni 29, huku mshindi akituzwa shilingi milioni 2 na kushiriki mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao.

Share This Article