Jaji Mkuu Koome ateua jopo la majaji watatu kuskiza kesi ya matozo ya nyumba

Dismas Otuke
1 Min Read

Jaji Mkuu Martha Koome ameteua jopo la Majaji watatu kuskiza na kuamua kesi, dhidi ya utekelezaji wa sheria ya matozo ya nyumba

Majaji walioteuliwa ni pamoja na:- Olga Sewe, John Chigiti na Josephine Mongare, ambao wamejukumiwa kusikiza kesi sita zinazopita sheria mpya ya matozo ya nyumba, huku moja ya kesi hiyo ikiwasilishwa na Maseneta 22 akiwemo Okiya Omtatah wa Busia.

Maseneta hao na wanaharakati wa haki za kibinadamu saba wanahoji baadhi ya vipengee kwenye sheria hiyo mpya ya nyumba, ikiwemo kipengee kinachoruhusu Kamishna mkuu wa mamlaka ya ushuru nchini KRA kukusanya matozo hayo.

Share This Article