Tume ya kuwajiri walimu nchini, TSC imetangaza kuwa itaanza mchakato wa kuwajiri walimu 20,000 kuanzia wiki ijayo.
Kulingana na mwenyekiti wa tume hiyo Jamleck Muturi, wanapanga kutoa tangazo la nafasi hizo za kazi wiki ijayo.
Idadi hiyo itafikisha elfu 50 jumla ya walimu watakaokuwa wameajiriwa na serikali ya Kenya Kwanza, baada ya kuwaajiri walimu 30,000 katika awamu ya kwanza wa kutoa elimu ya sekondari ya chini, JSS.
Walimu hao wataajiriwa kwa mktaba huku wakigharimu shilingi bilioni 4 nukta 6 ambazo ni sehemu ya shilingi bilioni 327 zilizotengewa Wizara ya Elimu katika bajeti ya mwaka 2023/2024.