Israel imetekeleza mashambuliz ya Makombora katika Mji Mkuu wa Iran, Tehran leo Ijumaa, huku milipuko mikubwa ikisikika.
Ikithibitisha kutekeleza mashambulizi hayo, Israel ilisema ilikuwa ikilenga maeneo ya nyuklia na vituo vya kijeshi.
Duru zinasema kuwa mashambulizi hayo pia yalilenga mji wa Kermanshah magharibi mwa Iran, ambapo wakazi walisema walisikia milipuko na kuona moshi mweusi ukipanda juu ya jiji.
Kupitia taarifa ya video, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel imeanzisha Operesheni ya kijeshi ya ‘Rising Lion’, inayolenga kurudisha nyuma tishio la Iran kwa “uhai wa Israel”.
Alisema kuwa Israel ililenga wanasayansi wa Iran kwamba mashambulizi “yataendelea kwa siku nyingi.
Kwa upande wake kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema mashambulizi hayo yanafichua asili mbaya ya Israeli, na kwamba Israeli imejiandalia hatma yenye uchungu.
Msemaji wa jeshi la Iran amesema kuwa Marekani na Israel zitalipa “gharama kubwa” kwa mashambulizi hayo, licha ya kwanza Marekani imesema haikuhusika katika shambulizi hilo.