Kusudi la Kenya ni kuandaa mashindano ya kimataifa, asema Waziri Namwamba

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri wa Michezo Ababu Namwamba

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba amesema Kenya iimedhamiria kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya kimataifa. 

Namwamba aliyasema hayo wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika kabla ya kuandaliwa kwa mashindano ya CECAFA ya wavulana wenye umri chini ya 18, CECAFA U-18 yaliyopangwa kufanyika katika kaunti za Kisumu na Kakamega kuazia Novemba 25 mwaka huu.

Aliyasema hayo wakati akiwa ameandamana na katibu wa wizara hiyo Mhandisi Peter Tum na Rais wa FKF Nick Mwendwa miongoni mwa maafisa wengine.

Kulingana na Namwamba, serikali ina kusudi la kukuza vipaji wakati ikiinadi nchi hii kama kivutio cha wengi.

Waziri alitoa wito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi na kuhudhuria mashindano ya CECAFA U-18 yaliyopangwa kufanyika katika kaunti za Kisumu na Kakamega.

Kulingana naye, mashindano hayo ni muhimu katika kuweka msingi wa kuunda timu madhubuti itakayoshiriki mashindano ya Kombe la Afrika mwaka 2027.

Mashindano hayo yataandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.

“Tunafurahi kuwataarifu kuwa ukuzaji wa vipaji nchini Kenya unaendelea vema. Tumetambua vipaji vya kupigiwa mfano katika pogramu mbalimbali kutoka gofu hadi soka,” alisema Namwamba.

 

Share This Article