Wakulima katika kaunti ya Mandera wanakadiria hasara kubwa kutokana na mafuriko yaliyosababisha uharibifu mkubwa katika kaunti hiyo.
Wakulima katika eneo la Mandera Mashariki, hasa katika mpango wa Border Point 1 ndio walioathiriwa zaidi huku ekari 35 za mimea zikiharibiwa.
Mimea kama vile kabichi, nyanya, mahindi na tikiti maji imeharibiwa na mafuriko.
Mohamed Arabey ni mmoja wa wakulima walioathiriwa. Anatoa wito kwa viongozi wa kaunti hiyo kutoa msaada wa kibinadamu, akielezea hali yao ya sasa ya ufukara.
Kwa upande wake, mkulima Mohamed Abdi anatoa wito kwa mashirika ya kilimo kutoa usaidizi kwa kuwaelimisha kuhusiana na namna ya kukabiliana na athari za mafuriko.
Mwakilishi wa Wanawake wa kaunti ya Mandera Ummulkheir ameelezea dhamira yake ya kuwasilisha mswada bungeni unaolenga kuwalinda wakulima na kuzuia uhariibifu zaidi.
Usombaji wa mimea katika mashamba yanyonyunyiziwa maji unaibua mashaka ya kutokea kwa uhaba wa chakula katika kaunti ya Mandera.