Manaibu Rais wa Benki ya Dunia na IFC kuhudumu kutoka Nairobi

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto wakati alipokutana na maafisa wa Benki ya Dunia katika Ikulu ya Nairobi

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika watahudumu kutoka jijini Nairobi, Kenya.

Rais William Ruto amepongeza uamuzi wa makamu hao kuhudumu kutoka Nairobi akisema hatua hiyo italifanya jiji la Nairobi kuwa kituo kikuu siyo tu katika kanda hii bali pia barani Afrika.

“Hii italifanya jiji letu kuwa kituo kikuu katika kanda yetu na barani Afrika, na jumuiya kubwa ya Benki ya Dunia ya wafanyakazi 870,” alisema Rais Ruto.

Aliyasema hayo alipokutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Victoria Kwakwa katika Ikulu ya Nairobi.

Kwakwa aliandamana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia humu nchini Qiamiao Fan.

Benki ya Dunia imekuwa mfadhili wa miradi ya maendeleo nchini Kenya kwa zaidi ya miaka 50.

“Imekuwa ikiunga mkono safari yetu ya kuwa nchi ya kipato cha kati ya daraja la juu kufikia mwaka 2030 kupitia mipango ya kupunguza umaskini na kuhamisha ustawi wa pamoja,”  aliongeza Rais Ruto.

Website |  + posts
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *