Zohran Mamdani achaguliwa Meya wa New York

Tom Mathinji
1 Min Read
Zohran Mamdani, achaguliwa Meya wa New York.

Zohran Mamdani ambaye ana asili ya Afrika, amechaguliwa Meya mpya wa Jiji la New York.

Mamdani aliye na umri wa miaka 34, ameungwa mkono na watu wengi licha ya kushtumiwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa kuwa Mkomunisti.

Meya huyo mpya ambaye alizaliwa Jijini Kampala,Uganda, alihamia New York Pamoja na familia yake  akiwa na umri wa miaka saba.

Kuchaguliwa kwake kwenye wadhifa huo kunamaanisha yeye ndiye Meya wa kwanza wa New York kutoka kusini mwa Asia.

Kwenye kampeni zake, Mamdani aliahidi ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,mabasi ya umma yasiyotoza nauli,kusimamishwa kwa kodi za nyumba na ulezi wa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Awali, Trump alikuwa ametishia kusitisha ufadhili kwa jiji la New York iwapo Mamdani angeshinda kiti hicho dhidi ya Andrew Cuomo ambaye alikuwa mgombeaji huru na Curtis Sliwa wa chama cha Republican.

Website |  + posts
Share This Article