Ipo haja ya kupanda miti inayoenda sambamba na hali ya hewa katika maeneo tofauti nchini ili kuwezesha ukuaji wa miti hiyo na pia kuafikia ndoto ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza katika hafla moja ya upanzi wa miti, Arnold Kipchumba ambaye ni Mkurugenzi wa kikundi cha kina mama cha Doing Good ameeleza kamba upanzi wa miti kulingana na hali za hewa husaidia pakubwa katika ukuaji wa miti hiyo na ni njia rahisi ya kuhakikisha miti mingi inayopandwa nchini inanawiri na kutonyauka.
Akielezea kwamba japo juhudi za upanzi wa miti nchini zimepamba moto kutokana na kampeni mbalimbali, bado miti mingi inayopandwa hunyauka kutokana na ukosefu wa elimu ya jinsi ya kupanda miti na kuikuza kufikia kiwango cha kutonyauka.
Usemi wake ulitiliwa nguvu na Mkurugenzi wa kituo cha teknolojia cha Konza alieelezea kwamba kupitia mbinu mpya, tayari zaidi ya miti milioni 5 imepandwa na kunawiri katika kituo hicho kupitia matumizo ya teknolojia za kisasa.
Taarifa ya Jonathan Musau