Zanzibar yatwikwa maandalizi ya CECAFA Senior Challenge

Dismas Otuke
1 Min Read

Zanzibar itakuwa mwenyeji wa makala ya mwaka huu ya fainali za kuwania kombe la CECAFA maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup.

Baraza kuu la CECAFA liliafikia uamuzi huo Alhamisi wakati wa kikako kikuu kilichoandaliwa katika mkahawa wa Pride Inn Paradise kaunti ya Mombasa.

Isayas Jira,ambaye ni makamu wa Rais wa he CECAFA na mwenyekiti wa kamati ya mashindano alitoa tangazo hilo Alhamisi.

Mashindano ya kombe la CEACAFA Senior Challenge yanarejea mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019 nchini Uganda.

Kando na kipute cha CECEFA,Zanzibar pia imeteuliwa kuandaa michuano ya kufuzu kwa mashindano ya Afrika kwa shule ukanda wa CECAFA, huku Uganda ikiwa mwenyeji wa mechi za CECAFA kufuzu kwa fainali za AFCON kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17, wakati Tanzania ikiandaa mechi za kufuzu kwa AFCON kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20.

Ethiopia itaandaa fainali za CECAFA kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 20 pamoja na michuano ya kufuzu kwa ligi ya Mabingwa kwa wanawake.

Website |  + posts
Share This Article