Misri wawahi tiketi ya AFCON mwakani baada ya kuiramba Guinea

Dismas Otuke
1 Min Read

Misri almaarufu The Pharoes, waliwahi tiketi ya fainali za kombe la Afrika mwakani baada ya kutoka nyuma na kuwabwaga Guinea magoli 2 -1, katika mechi ya kundi D raundi ya tano iliyopigwa Jumatano usiku kiwarani Marrakech nchini Morocco.

Serhou Guirassy aliiweka Guinea uongozini kwa goli la dakika ya 26, kabla ya Misri ambao ni mabingwa mara 10 wa Afrika kusawazisha kupitia kwa mchezaji Mahammud Trezequet aliyeungisha pasi ya nahodha Mohammed Salah dakika ya 42.

Mustafa Mohammed alifunga kazi kwa bao la dakika ya 79 na kuhakikisha Misri wanatinga kipute cha mwakani nchini Ivory Coast wakiongoza kundi D kwa alama 12 ,tatu zaidi ya Guinea .

Guinea pia watafuzu rasmi mwishoni mwa juma endapo Malawi na Ethiopia watatoka sare .

Mataifa manane yamefuzu kwa patashika ya 34 ya AFCON itakayoandaliwa kati ya Januari 13 na Februari 11 mwakani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *