Zambia yarejelea zoezi la kuhesabu kura

Kulingana na tume hiyo, tisho la kiusalama lililokuwa limeripotiwa hapo awali kuhusiana na mchakato wa uchaguzi, sasa umedhibitiwa.

Tom Mathinji
1 Min Read
Zambia yarejelea zoezi la kuhesabu kura.

Tume ya Uchaguzi nchini Zambia imetangaza kurejelea shughuli ya kuhesabu kura za Urais na Ubunge, baada ya kusitishwa kutokana na madai ya ghasia na wizi wa karatasi za kupiga kura.

Kulingana na tume hiyo, tisho la kiusalama lililokuwa limeripotiwa hapo awali kuhusiana na mchakato wa uchaguzi, sasa umedhibitiwa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Mwangala Zoloumis, alitangaza kurejelewa kwa zoezi hilo bila kusema kuwa iwapo karatasi za kura zilizoibiwa zitaathiri matokeo ya uchaguzi huo.

Rais Hakainde Hichilema, anatafuta muhula wa pili kwenye uchaguzi huo, lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Brian Mundubile mwenye umri wa miaka 55.

Mundubile anagombea Urais kwa tiketi ya chama cha NRPUP.

Matangazo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumatatu.

 

Share This Article