Watu 20 wafariki kwenye tetemeko la ardhi Indonesia

Tetemeko hilo lilisababisha wanavijiji 2,000 katika eneo la Nagekeo regency, kuhama makwao kutafuta makazi ya muda.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 20 wafariki kwenye tetemeko la ardhi Indonesia.

Takriban watu 20 wamefariki baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.7  kukumba Indonesia, Jumamosi asubuhi.

Kulingana na mamlaka nchini humo, watu kadhaa pia walijeruhiwa kwenye tetemeko hilo lililotokea kusini mwa nchi hiyo, na kusababisha uharibifu wa miundombinu.

Watu wawili hawajulikani waliko, huku wananchi kwenye maeneo ya pwani wakishauriwa kuhamia maeneo ya juu.

Mamlaka ilikuwa imetoa onyo la kutokea kwa tsunami, lakini baadaye Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ikasema hakuna dalili zozote kwenye viwango vya bahari na kuondolea mbali hofu ya tsunami.

Idara ya taifa ya kukabiliana na majanga, ilipelekea ndege aina ya helikopta kusaidia katika operesheni ya dharura, ikiwa kuwahamisha watu.

Tetemeko hilo lilisababisha wanavijiji 2,000 katika eneo la Nagekeo regency, kuhama makwao kutafuta makazi ya muda.

TAGGED:
Share This Article