Klabu ya Zamalek ya Misri, ndio mabingwa wa kombe la shirikisho la soka barani Afrika, baada ya kuwalaza RS Berkane ya Morocco kwa goli Moja Jumapili usiku mjini Cairo.
Zamalek walitawala mechi hiyo kutoka mwanzo huku Ahmed Hamdi akipachika goli dakika ya 23.
Ngoma hii ya awamu ya pili, ilisakatwa ugani Cairo mbele ya mashabiki lukuki waliobeba mabango na kuruka Kwa furaha baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Kwenye mukondo wa kwanza wa fainali hiyo kule Morocco, RSB Berkane walivuna ushindi wa 2-1.
Bao hili la ugenini ndilo liliwapa Zamalek ubingwa baada, ya mechi kumalizikia sare ya mabao 2-2 Kwa jumla.
Hii ni mara ya pili kutwaa taji hilo baada ya kulinyakua mwaka 2019.
Misri huenda ikabugia mstaji yote mawili huku mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Al Ahly, wakiwatumbuiza Esperance ya Tunisia Jumamosi hii katika marudio ya fainali.
Timu zote zitoka sare kappa katika duru ya kwanza Jumamosi iliyopita mjini Tunis.