Watu zaidi ya 100 wakufa maji Nigeria

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu kadhaa wanaaminika kufa maji huku wengine wengi wakitoweka baada ya mashua iliyokuwa imewabeba kuzama kwenye mto Niger.

Baadhi ya ripoti zinaashiria kwamba wasafiri hao walikuwa wakirejea kutoka kwa hafla ya harusi.

Mashua hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka jimbo la Niger kuelekea lile la Kwara kwa mujibu wa maafisa.

Haijabainika kilichosababisha ajali hiyo.

Kulingana na mkuu wa Pategi, eneo ambako mkasa huo ulitokea, zaidi ya watu 150 wamethibitishwa kuaga dunia.

Ajali kama hizo hutokea mara kwa mara nchini Nigeria.

Mwezi uliopita, watu 14 waliaga dunia baada ya mashua kuzama kwenye jimbo jirani la Sokoto.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *