Ruto aongoza Wakenya kutoa heshima za mwisho kwa Raila bungeni

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekuwa miongoni mwa Wakenya waliojitokeza katika majengo ya Bunge mapema Ijumaa, kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Mazishi ya kitaifa hujumuisha mwili huo kulazwa katika majengo ya bunge ili umma wautazame na kutoa heshima za mwisho.

Ruto akiandama na mkewe Rachael Ruto,familia ya hayati Raila ikiongozwa na mjane mama Ida Odinga waliutazama mwili huo .

Raila aliyefariki Jumatano wiki hii akiwa na umri wa miaka 80 atazikwa nyumbani kwake Bondo siku ya Jumapili.

Website |  + posts
Share This Article