Ibada ya Raila yaanza uwanjani Nyayo

Dismas Otuke
1 Min Read

Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo mapema Ijumaa kuhudhuria ibada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Rais William Ruto na viongozi wakuu serikalini, viongozi wa kimataifa akiwemo Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamud, Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, Makamu Rais wa Tanzania Philip Isdor Mpango na Mabalozi wamejitokeza kutoa heshima za mwisho.

Mwili wa hayati Raila ukiwe umebebwa na gari la kijeshi umezungushwa katika uwanja wa Nyayo ili kuruhusu wananchi kutoa heshima zao za mwisho.

Ibada hiyo inaongozwa na kanisa la Kianglikana.

Website |  + posts
Share This Article