Zaidi ya washiriki 1,000 watimka mbio za Karura

Mbio za Jumapili zilishirikisha vitengo vya nusu marathoni,kilomita 10,kilomita 5 na kilomita  ni pia zilitoa uhamisisho kuhusu utunzaji mazingira.

Dismas Otuke
1 Min Read
BCS_Photography

Zaidi ya washiriki 1,000 walijitokeza Jumapili kushiriki mbio za msitu wa Karura,ambazo ni mojawapo wa maandalizi ya mbio za Standard Chartered Nairobi Marathon mwezi ujao.

Mbio za Jumapili zilishirikisha vitengo vya nusu marathoni,kilomita 10,kilomita 5 na kilomita  ni pia zilitoa uhamisisho kuhusu utunzaji mazingira.

Washiriki pia walipata fursa ya kutazama mbio za Berlin Marathon kupitia kwa runinga zilizotawaliwa na wanariadha wa kutoka Ethiopia.

Makala ya 23 ya mbio za Standard Chartered Nairobi Marathon yataandaliwa tareehe 25 mwezi ujao katika bustani ya  Uhuru Gardens.

Mbio za mwaka huu zimewavutia wanaroadha wapatao 30,000 kutoka mataifa 102 wakiwemo wanariadha 400 wa kulipwa.

Share This Article