Maandalizi kwa uapisho wa Mfalme Edward Rukidi Nyabongo wa Tooro yanoga

Uapisho huo utafanyika katika Kasri la Karuziika,hafla inayotarajiwa kuhudhuriwa na kuongozwa na serikali ya Uganda.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maandalizi ya kuapishwa kwa Edward Rukidi Nyabongo kuwa Mfalme wa Tooro nchini Uganda, yameshika kasi huku hafla ya uapisho wake ikiratibiwa kuandaliwa  Jumanne Septemba 29.

Rukidi atamrithi Mfalme Oyo Nyimba aliyefariki mwezi uliopita akipokea matibabu nchini Marekani.

Rukidi ambaye ni mwanahabari alichafuliwa kuwa mfalme na kamati ya wazee kufuatia kifo cha mtangulizi wake.

Uapisho huo utafanyika katika Kasri la Karuziika,hafla inayotarajiwa kuhudhuriwa na kuongozwa na serikali ya Uganda.

Ufalme wa Tooro ni miongoni mwa Falme tano za kitamaduni ambazo bado zinatambuliwa na serikali ya Uganda.

Share This Article