Moto mkubwa wazuka wananchi wakiteka mafuta kutoka kwa lori, Mayanja

Moto huo umesababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara hiyo huku maafisa wa uokoaji kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu wakifika kuwasaidia majeruhi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Moto mkubwa umezuka katika kijiji cha Mayanja Jumapili alasiri baada ya lori la mafuta kupata ajali na kupinduka katika barabara ya Bungoma-Malaba.

Inaaminika moto huo ulizuka baada ya mamia ya raia kufika eneo la ajali na kuanza kuteka mafuta kwa kutumia mitungi.

Moto huo umesababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara hiyo huku maafisa wa uokoaji kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu wakifika kuwasaidia majeruhi.

Mkasa huo umetokea karibu na shule ya upili ya Paul Boit High kwenye barabara kuu ya Eldoret-Turbo.

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya watu watatu kufariki na wengine 23 kupata majeraha ya moto baada ya lori la mafuta kupata ajali na kulipuka moto wakati wakazi wakijaribu kuteka mafuta.

Share This Article