Zaidi ya wanafunzi milioni tatu unusu kutahiniwa mwaka huu

Dismas Otuke
1 Min Read

Zaidi ya wanafunzi milioni tatu unusu wamesajiliwa kufanya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu itakayoanza mwezi Oktoba ikiwemo mtihani wa KPSEA,KCPE na KCSE.

Idadi ya mwaka huu itakuwa ya juu zaidi katika historia ya mitihani ya kitaifa.

Takriban watahiniwa milioni moja watafanya mtihani wa kidato cha nne K.C.S.E,milioni 1 nukta 2 wakalie mtihani wa elimu ya mtaala wa umilisi CBC maarufu kama KPSEA  na wengine milioni 1 nukta 4 watahiniwe mtihani wa darasa la nane K.C.P.E.

Wanafunzi zaidi ya laki tatu wakaofanya mitihani ya mwaka huu ni watu wazima huku wengine wakiwa wanafunzi wa kibinafsi.

Mtihani wa K.C.P.E utaandaliwa kati ya Oktoba 27 na Novemba mosi nayo K.C.S.E ifanyike baina ya Oktoba 23 na Novemba 24 huku KPSEA ikianda Octoba 30 na kukamilika Novemba 1.

Share This Article