Zaidi ya maafisa 500 wa DCI wapandishwa cheo

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa 500 wa DCI wapandishwa cheo.

Maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI, wamehimizwa kutekeleza majukumu yao kwa maadili na kwa kuzingatia sheria.

Hayo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa idara ya DCI Mohamed Amin, alipoongoza hafla ya kuwapandisha vyeo zaidi ya maafisa wa DCI katika chuo cha mafunzo cha Magadi.

katika hafla hiyo maafisa 360 wa DCI walipandishwa cheo hadi Konstabo, huku maafisa 152 wakipandishwa ngazi kuwa Sajenti.

Amin alimpongeza Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome, kwa kuamini uwezo wa DCI kutoa mafunzo kwa maafisa wake na kuwapandisha cheo, akisema hatua hiyo imeipa motisha idara hiyo kuangazia maswala muhimu ya mafunzo yanayohusiana na shughuli zao za kila siku.

Mkurugenzi wa Operesheni katika idara hiyo Richard Mwaura, aliwataka maafisa hao kudumisha utaalam, akiwakumbusha kuwa wananchi wanatarajia huduma bora kutoka kwao.

Mafunzo hayo yaliyoanza wiki 17 zilizopita, yalilenga kunoa makali ya uwezo wa uchunguzi wa maafisa hao, huku wakipokea ujuzi wanapoingia katika nyadhifa za uongozi.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *