Yanga yamnyofoa mnyama Simba ,derby ya Kariakoo

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga SC, wamepata haki za kujigamba baada ya kumpiga mnyama Simba bao moja komboa ufe, kwenye derby ya Kariakoo iliyosakatwa Jumamosi jioni katika uga wa kitaifa wa Benjamin Mkapa.

Mpia Nzengeli alifyatua kombora la pekee la dakika ya 89 na kuwanyanyua mashabiki wa timu ya Mwanainchi, huku wale wa Wekundu wa Msimbazi wakiinamisha vichwa baada ya kipenga cha mwisho.
Ushindi huo  umeipasha Yanga hadi nafasi ya pili kwa alama 15,moja nyuma ya viongozi Singida Black Stars ,huku Simba wakipokea kichapo cha kwanza na kusalia nambari nne kwa pointi 13.
Share This Article