Yanga yaikwatua Medeama kwa Mkapa

Dismas Otuke
1 Min Read

Yanga walisajili ushindi wa kwanza katika kundi D kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika, baada ya kuwalemea Medeama kutoka Ghana mabao matatu  siku ya Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wenyeji walichukua uongozi kunako dakika ya 33 kupitia kwa  kiungo wa Ivory Coast Paedo Zouzoua, kabla ya Bakari Mwamnyeto na Yahya Mudathir kuongeza moja kila mmoja katika kipindi cha pili .

Ushindi huo unafufua mataumaini ya Yanga kufuzu kwa hatua ya mwondoano wakishikilia nafasi ya pili kwa alama 5.

Share This Article