Timu ya Young Africans ya Tanzania ilianza vibaya mechi za makundi ikiambulia kichapo cha mabao 2 kwa bila kutoka kwa wageni Al Hilal Omdurman ya Sudan, katika mechi ya kundi A iliyosakatwa katika uwanja uwanja wa Chamazi.
Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania bara wanakabiliwa na hatari ya kubanduliwa mapema katika kipute hicho ,huku wakiratibiwa kuwazuru MC Alger ya Algeria katika mechi ya pili Disemba 7.
Ushinde huo ulikuwa katika mechi ya kwanza ya kocha mpya wa Yanga Sead Ramovic aliyeshika hatamu, baada ya Miguel Gamondi kuonyeshwa mlango kutokana na msururu wa matokeo mabovu tangu kuanza kwa msimu huu.