Serikali imefikia lengo lake la kuweka mtandao wa faiba nchini ndani ya mwaka wa kwanza wa utawala wa serikali ya Kenya Kwanza chini ya uongozi wa Rais William Ruto.
Haya yamesemwa mapema leo Jumatatu na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali Eliud Owalo, alipozindua ripoti ya mwaka mmoja ya utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza.
Kulingana na Owalo, wizara yake imeweka faiba umbali wa zaidi kilomita 5,200 na kupitisha kiwango kilomita 5,000 zilizokadiriwa.