Wizara ya Ulinzi kukabidhi bustani ya Uhuru kwa serikali ya kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Ulinzi Aden Duale.

Waziri wa ulinzi Aden Duale, amesema atakabidhi bustani ya Uhuru kwa serikali ya kaunti ya Nairobi, baada ya kukamilika kwa ukarabati wa bustani hiyo.

Akijibu maswali kutoka kwa Maseneta, Duale alisema kazi iliyosalia ni asilimia nane, inayojumuisha uunganishaji wa maji na mabomba ya kupitisha majitaka.

“Nitakabidhi bustani hiyo siku ya Alhamisi saa tatu asubuhi kwa serikali ya kaunti ya Nairobi, usimamizi wa bustani sio jukumu letu. Hata hivyo wizara ya ulinzi imewaruhusu wananchi kutumia bustani hiyo kwa hafla tofauti,” alisema waziri Duale leo Jumatano.

Bustani ya Uhuru, imekuwa ikikarabatiwa tangu mwezi Septemba mwaka 2021, shughuli iliyotekelezwa na vikosi vya ulinzi nchini KDF, chini ya iliyokuwa huduma ya usimamizi wa Nairobi NMS, kwa lengo la kupandisha hadhi bustani hiyo kufikia viwango vya Kimataifa.

Kaunti ya Nairobi itasimamia bustani ya Uhuru na ile ya Central, baada ya ukarabati kukamilika.

TAGGED:
Share This Article