Wizara ya uchukuzi yaongeza marufuku wa kuwatathmini madereva kwa miezi mitatu

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya uchukuzi imeongeza muda wa marufuku ya kuwatathmini madereva nchini kwa kipindi cha miezi mitatu.

Katika taarifa ya waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen siku ya Ijumaa ,utathmini kwa  madereva wa magari ya usafiri wa umma na malori umeongezwa kwa miezi mitatu zaidi kupisha majadiliano baina ya wadau wa sekta ya uchukuzi.

Utathimini wa leseni kwa madereva wa magari ya usafiri wa umma na malori ya mizigo uliohitaji kupokea mafunzo upya ulizua tumbo joto ,maderva wakigoma kupinga sheria hiyo.

Share This Article