Wizara ya utamaduni, sanaa na michezo nchini Tanzania, imeungana na wengine kumwomboleza mwigizaji nguli wa kipindi cha “Huba” Grace Mapunda, maarufu kama Tessa.
Wizara hiyo inatoa ujumbe wa pole kwa familia, marafiki na wahusika wa tasnia ya uigizaji kwa msiba uliowafika.
The Ministry extended its condolences to the family, friends, and members of the film industry across the country on the loss of their beloved.
Ujumbe huo ulichapishwa kwenye akaunti ya mtandao wa Instagram ya wizara hiyo.
Grace anaripotiwa kuaga dunia mapema Jumamosi Novemba 2, 2024 katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa anapokea matibabu.
Mwelekezi wa kipindi cha Huba Aziz Ahmed alielezea kwamba Grace alilazwa hospitalini humo Oktoba 31, 2024 baada ya kupata matatizo ya kupumua.
Alisema pia kwamba mwigizaji huyo aliugua kwa muda mrefu lakini katika siku za hivi karibuni alionekana kupata nafuu kiasi cha kurejelea kazi zake za kawaida.
Mwigizaji huyo hata hivyo aligonjeka na kupelekwa hospitalini siku hiyo ambapo alifariki jana asubuhi.
Aziz aliahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu msiba huo wa Grace kama vile mipango ya mazishi.
Watu maarufu nchini Tanzania wamekuwa wakifika nyumbani kwa Grace eneo la Sinza jijini Dar es Salaam, kuomboleza na familia.