Wizara ya Nishati na Petroli imewateuwa Wakurugenzi Wakuu wapya kwenye mashirika yake matatu.
Tom Odhiambo Imbo, ameteuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya usambazaji wa umeme (KETRACO), huku Stephen Kipsang Busieney akichukua hatamu katika kampuni ya Geothermal Development Company Limited (GDC).
Kwa upande mwingine, mhandisi Edward Mwirigi Kinyua, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA).
Waziri wa Nishati na Petroli Opiyo Wandayi, aliidhinisha uteuzi huo ambao unatekelezwa mara moja baada ya kukamilika kwa mchakato wa bodi husika kuambatana na sheria na miongozo ya uajiri.
Wandayi aliwapongeza walioteuliwa ambao wanatarajiwa kuimarisha sekta ya Nishati na Petroli ya taifa hili.