Wizara ya Elimu yatakiwa kutenga vyumba vya kuwanyonyeshea watoto

Martin Mwanje
1 Min Read

Chama cha Walimu Wanawake Nchini, KEWOTA kimetoa  wito kwa Wizara ya Elimu kuwatengea walimu wanawake vijana vyumba maalum vya kuwanyonyeshea watoto. 

Chama hicho kinasema hatua hiyo itawawezesha kuwanyonyesha watoto wao wachanga na kutangamana nao kiasi punde watoto hao wanapoletwa na walezi wao.

KEWOTA hushughulikia maslahi ya walimu kwa kuboresha viwango vya maisha vya wanawake walimu kwa kutoa fursa za ustawi wa kitaalam, kiuchumi na kibinfasi.
Kilifanya mkutano wake wa kila mwaka ambapo kilijadili masuala wanayokumbana nayo walimu wanawake na yanayopaswa kuangaziwa na serikali.
Mweka Hazina wa Kitaifa wa chama hicho Jacinta Ndegwa akizungumza wakati wa mkutano huo, alisema kuna haja kwa shule zote kuwa na chumba maalum cha walimu wanawake vijana kuwanyonyeshea watoto wao.
Alitaja hali ya kiakili ya walimu ambapo wanakumbana na changamoto za kiakili bila kutambuliwa, dhuluma za kijinsia wakiwa nyumbani na shuleni na namna ya walimu kuanza kuwekeza kuwa baadhi ya changamoto ambazo zinapaswa kuangaziwa.
Website |  + posts
Share This Article