Wizara ya uchukuzi na barabara kupitia kwa waziri Kipchumba Murkomen imelaani uharibifu uliotekelezwa leo kwenye miundomsingi barabarani wakati wa maandamano.
Kupitia taarifa kwa vyumba vya habari jioni ya leo, Murkomen alisema kwamba wameiomba afisi ya upelelezi wa jinai DCI itekeleze uchunguzi ili kuhakikisha kwamba walioharibu mali ya umma na ambao walinakiliwa na kamera za CCTV na za wanahabari wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kisheria.
Murkomen anataka waandalizi wa maandamano siku za usoni wahakikishe wafuasi wao hawaharibu mali la sivyo wao wenyewe watagharamia uharibifu utakaotekelezwa.