Wizara ya Afya yatoa mitambo ya kidijitali 548 kwa hospitali za umma Uasin Gishu

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Afya ilitoa mitambo ya kidijitali 548 kwa hospitali 131 za umma katika kaunti ya Uasin Gishu katika juhudi za kueneza utoaji huduma za afya kidijitali.

Waziri wa Afya Aden Duale akiongoza hafla hiyo siku ya Jumatano alisema hatua hiyo inalenga kuharakisha utoaji huduma na kumaliza utoaji huduma duni kwa wagonjwa.

Aidha Duale alitangaza kuwa kaunti ya Uasin Gishu itanufaika kwa uboreshaji wa mitambo ya kutoa huduma za afya ikiwemo ile ya CT scans, X-rays, mammograms na mashine nyingine za kuokoa maisha.

Website |  + posts
Share This Article