Wizara ya Afya kutoa chanjo dhidi ya Polio

Tom Mathinji
1 Min Read
Watoto milioni 3.8 kuchanjwa dhidi ya ugonjwa wa Polio.

Wizara ya afya inalenga kuanzisha kampeini ya siku tano ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza wa polio.

Hatua hiyo imeafikiwa baada ya kuripotiwa visa 5 vya ugonjwa huo katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma na katika mtaa wa Kamukunji jijini Nairobi.

Kulingana na wizara hiyo, zoezi hilo litakaloanza Oktoba 2-6, linalenga kuwachanja watoto milioni 3.8 walio na umri wa miaka 10.

Kupitia mtandao wa X Jumatatu asubuhi, wizara hiyo ilisema ni jukumu lake kuhakikisha kila mtoto hapa nchini analindwa kwa kupewa chanjo hiyo.

“Serikali ya Kenya imejitolea kuangamiza ugonjwa wa polio hapa nchini, na inahakikisha kila mtoto analindwa kwa kupatiwa chanjo,” ilisema wizara hiyo.

Akizungumza leo Jumatatu na wanahabari, Katibu wa afya ya umma Mary Muthoni, alisema chanjo hiyo itatolwa katika kaunti tisa zilizo katika hatari ya chamko la ugonjwa huo.

Kaunti hizo ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Busia, Bungoma, Turkana, Pokot magharibi, Marsabit, Trans nzoia na Machakos.

Wazazi na walezi walihimizwa kuhakikisha watoto wao wanachanjwa.

Share This Article