Winfrida Moseti amaliza wa pili Tokyo Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Winfrida Moseti wa Kenya amemalzia wa pili katika makala ya mwaka huu ya mbio za Tokyo Marathon, zilizoandaliwa mapema leo nchini Japan.

Moseti alitumia saa 2 dakika 16 na sekunde 56 kuzikamilisha nyuma ya Sutume Kebede, kutoka Ethiopia aliyeibuka mshindi kwa saa 2 dakika 16 na sekunde 31.

Hawi Feysa pia wa Ethiopia alichukua nafasi ya tatu huku Wakenya wengine Magdalyne Maasai na Rosemary Wanjiru, wakiambatana katika nafasi za nne na tano katika usanjari huo.

Vincent Kipkemboi wa Kenya alichukua nafasi ya tatu katika mbio za wanaume kwa saa 2 na dakika 4,nyuma ya Tadese Takele na Daresa Geleta wa Ethiopia walionyakua nafasi za kwanza na pili mtawalia.

Titus Kipruto na Geofrey Toroitich wa Kenya walichukua nafasi za nne na sita mtawali

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *