Willy Paul asema alitilia maanani ushauri wa Wakenya

Wakosoaji wa Willy Paul waliotoa maoni baada ya tukio la Raha Fest wapendekeza awe na wasimamizi kwani angekuwa nao, hangepitia aliyoyapitia.

Marion Bosire
2 Min Read
Willy Paul, Msanii wa muziki wa Kenya

Mwanamuziki Willy Paul amesema kwamba alisikia na kutiilia maanani ushauri wa Wakenya kuhusu haja ya kuwa na msimamizi au wasimamizi.

Amesema hayo kupitia Instagram ambapo aliandika, “Wakenya wenzangu, mwaka huu, nimetiilia maanani ushauri wenu na katika muda wa siku chache, nitawatangazia kundi langu, usimamizi wangu.”

Msanii huyo ambaye mwisho wa mwaka jana alihusika katika zogo la tamasha la Raha Fest, amewashukuru wakenya kwa maenzi ambayo wamekuwa wakimwonyesha katika muda wa miaka kadhaa.

Kulingana naye, mapenzi hayo yamemlazimu awasikilize na alainishe mambo katika kazi yake. “Sasa tuungane tuufanye mwaka huu uwe bora zaidi.” aliandika Willy Paul.

Wakosoaji wa Willy Paul waliotoa maoni baada ya tukio la Raha Fest wapendekeza awe na wasimamizi kwani angekuwa nao, hangepitia aliyoyapitia.

Pozee anaendelea kutangaza tamasha lake litakalofanyika Februari 14, 2025 katika eneo la KICC jijini Nairobi ambapo anahimiza wapenzi wa sanaa yake wanunue tiketi.

Katika chapisho jingine Pozee alimtupia maneno Mwijaku mtangazaji wa Tanzania aliyesema kwamba iwapo hangeomba msamaha kwa Diamond, hangeona mwaka mpya wa 2025.

“Walisema sitaona 2025, Umetenda tena baba, mwaka mwingine mpya na fursa nyingine ya kulainisha mambo na kuaibisha maadui wa maendeleo.” aliandika Pozee.

Baada ya mvutano wa raha Fest ambapo Willy aliingia jukwaani kabla ya Diamond kuishia kwa hatua ya Diamond kukataa kutumbuiza na hivyo kutupiwa maneno na wengi, Mwijaku alimlaumu Pozee huku akimlaani kwamba hangeona mwaka mpya.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *