Shirika la afya ulimwenguni W.H.O limeidhinisha chanjo ya pili kwa watoto dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambayo ni nafuu,kati ya shilingi 300 na 600.
Chanjo hiyo ya R21 ni ya pili kuidhinishwa baada ya ile ya RTS,S/ASO1 iliyokuwa imeidhinishwa kutumika mwezi Julai mwaka huu.
Watoto 4800 walitumika kwenye majaribio ya tatu ya chanjo hiyo yaliyofanywa katika mataifa manne ya Afrika ikiwemo Kenya,Mali,Burkina Faso na Tanzania.