Spika wa bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula amewasili mjini Juba nchini Sudan Kusini kwa kikao cha Maspika wa mabunge ya Afrika Mashariki kitakachoandaliwa Alhamisi.
Spika wa bunge la Seneti Amason Kingi anawakilishwa na Seneta mteule Veronica Maina.
Maspika wa mabunge sita ya Afrika Mashariki wanahudhuria kikao hicho.
Muungano wa Maspika wa Afrika Mashariki ulibuniwa mwaka 2008 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa mabunge ya ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.