Wetang’ula aonya dhidi ya siasa za chuki nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, ameelezea masikitiko yake kuhusu ongezeko la visa vya  kihuni kwenye mikutano ya kisiasa akionya kuwa inahatarisha demokrasia huku taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuuu wa mwaka ujao.

Wetangula amewataka wanasiasa na wafuasi wao kuendesha kampeini za amani na kuhimiza kuvumiliana.

Alivitaka vyombo vya kiusalama kuilingilia kati na kukabiliana na wale wanaojihusisha na visa vya uhuni kwenye mikutano ya kisiasa.

Spika alisema haya Jumapili alihudhuria ibada katika kanisa la St Mary’s Catholic ,Siyoi,eneo biunge la Kapenguria kaunti ya West Pokot.

Share This Article