Wetang’ula aitaka serikali kutuma wanajeshi Baragoi

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, ameitaka serikali kuwatuma wanajeshi wa KDF eneo la Baragoi kaunti ya Baringo, kukabiliana na utovu wa usalama.

Utovu wa usalama umekithiri eneo hilo siku zilizopita na nyakati nyingine kusababisha maafa na wizi wa mifugo wasiohesabika.

Wetang’ula amekariri kuwa maafisa wa KDF wanapaswa kukita kambi Baragoi ili kukabiliana na wizi wa mifugo na kuhakikisha mifugo walioibwa wamerejeshwa.

Spika aliyasema hayo alipohudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa Katoliki la
Maralal, alikoongoza hafla ya mchango wa pesa.

Aliahidi kuishinikiza serikali kutoa usalama wa kutosha katika kaunti ya Samburu, ambayo pia imekabiliwa na ukosefu wa usalama kwa muda mrefu.

Share This Article