Wetang’ula abuni kamati ya kutayarisha mazishi ya mbunge Kiaraho

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula  amebuni kamati itakayoandaa mipango ya mazishi ya Mbunge wa Ol Kalou David Njuguna Kiaraho, aliyefariki mapema Jumapili akipokea matibabu.

Kamati hiyo itaongozwa na Mbunge wa Kinangop Kwenya Thuku, akisaidiwa na mwakilishi wa kike wa Nyandarua Faith Gitau.

Marehemu Kiaraho alichaguliwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2013 ,kwa tiketi ya chama cha The National Alliance (TNA) .

Kiaraho alichaguliwa kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwaka 2022 ,akimbwaga mgombeaji wa chama tawala cha United Democratic movement (UDA) ,katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.

Share This Article