Ujerumani na Italia kubaini mbivu na mbichi huku mwondoano wa Euro ukianza

Dismas Otuke
1 Min Read

Hatma ya wenyeji Ujerumani na mabingwa watetezi Italia kufuzu  fainali za  kipute cha bara Ulaya(Euro)  itabainika  leo,watakapocheza mechi za raundi ya 16 bora .

Kwenye mechi ya kwanza, Italia itakabana koo na Uswizi ugani Olympiastadion Berlin kisha Ujerumani imenyane na Denmark uwanjani Signal Iduna Park.

Hata hivyo,Ujerumani huenda ikakosa huduma za beki matata wa kati Antonio Rüdiger, aliye na jeraha na Jonathan Tah aliye na kadi mbili za njano.

Nafasi zao zikachukuliwa na Waldemar Anton na Nico Schlotterbeck.

Vile vile, Denmark itamkosa beki mkabaji Morten Hjulmand aliye na kadi mbili za njano huku  pengo hilo litajazwa na Christian Norgaard au Mathias Jensen.

Italia nao watakosa huduma za beki Riccardo Calafiori anayetumikia adhabu ya kadi mbili za njano nafasi hiyo ikitwaliwa na Gianluca Mancini .

Shida hiyo pia inamwandama Silvan Widmer wa Uswizi na huenda Leonidas Stergiou akawajibika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *