Wenyeji Morocco wamejumuishwa kundi gumu la A katika fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) mwaka ujao.
Morocco wamejumuishwa pamoja na Zambia,Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Senegal.
Kundi B linasheheni Nigeria,Tunisia,Algeria na Botswana huku Afrika Kusini,Ghana ,Mali na Tanzania zikijumuishwa kundi C.
Kipute cha WAFCON kitaandaliwa kati ya Julai mosi na 26 maka ujao nchini Morocco baada ya kuahirishwa mwaka jana kutokana na michezo ya Olimpiki.