Wenyeji Australia wamefuzu kwa raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia baada ya kuwagaragaza mabingwa wa Olimpiki Canada mabao 4 kwa bila katika mchuano wa kundi B uliopigwa mjini Melbourne Jumatatu.
Hayley Raso alipachika magoli mawili kabla ya Mary Fowler na Steph Catley kutikisa nyavu kwa Matildas.
Australia wameongza kundi B kwa pointi 6, moja zaidi ya Nigeria iliyomaliza ya pili baada ya kutoka sare tasa na Ireland.