Wema Sepetu asema hataki kufanaishwa!

Ameghadhabishwa na hatua ya watumiaji mitandao nchini Tanzania kufananisha safari yake ya ujauzito na kujifungua na ile ya Zuchu.

Marion Bosire
1 Min Read

Mrembo wa Tanzania Wema Sepetu amesema kamwe hataki kufananishwa na watu wengine. Alitangaza hayo kupitia Instagram ambapo alichapisha picha zake za hivi punde akijirejejelea kama ‘tasa’.

“Tasa La Kwenda hilo… Mgumba flani Amazing… Ambaye hawezi kuja kupata mtoto hata iweje. Nimekubali vyote. Acheni tu kunifananisha,” aliandika chini ya picha zinazomwonyesha akiwa na furaha.

Hasira za mwanadada huyo ambaye ni mwigizaji zinaaminika kutokana na hatua ya watumiaji mitandao nchini Tanzania kufananisha safari yake ya ujauzito na kujifungua na ile ya Zuchu.

Video za wawili hao wanaodaiwa kujifungulia kwenye hospitali moja zilichapishwa mitandaoni ambapo wote wanafanya mazoezi ya kabla ya kujifungua wakiwa na waume zao.

Wema kwa upande wake anaonekana akiwa mchangamfu akiruka ruka huku akiwa ameshikwa mkono na Whozu huku Zuchu akionekana kuongeza uzani wa mwili maradufu, amefura hadi usoni, anatembea pole pole akisaidiwa na Diamond.

Kulingana na maoni wengi wanasema Wema hakubeba mimba ila alibebewa na mtu huku Zuchu akibeba mimba kweli lakini Wema amesema, “Ilikuwa feki. Mmepata vya Ukweli basi niacheni.”

Share This Article