Weasel kutohudhuria matamasha ya Krismasi

Kaka huyo mdogo wa Jose Chameleone ndiye aliandamana na mwanamuziki huyo hadi Marekani kwa matibabu zaidi.

Marion Bosire
1 Min Read

Weasel Manizo mwanamuziki wa Uganda ambaye jina lake halisi ni Douglas Mayanja, ambaye pia ni kaka mdogo wa Jose Chameleone hatahudhuria matamasha aliyokuwa amepangiwa kutumbuiza msimu wa Krismasi.

Kulingana na taarifa kutoka kwa usimamizi wa msanii huyo, Weasel amelazimika kutokuwepo kwenye matamasha hayo kwa sababu alisafiri ghafla kuelekea Marekani.

Yeye ndiye alimpeleka Chameleone nchini Marekani kwa ajili ya kupokea matibabu.

Ujumbe wa wasimamizi wa Weasel ulimalizika kwa kuwataka mashabiki zake kuwatakia kaka hao wawili mema wakati huu mgumu huku ukiwatakia Krismasi njema.

Chameleone alikuwa amelazwa kwenye hospitali moja jijini Kampala ambapo rafiki yake Juliet Zawedee alimzuru na kuahidi kumpeleka Marekani kwa matibabu zaidi.

Kulingana na video na picha zilizochapishwa mitandaoni, Juliet aliandamana na kaka hao wawili kwa safari hiyo ya Marekani.

Katika taarifa aliyoaichapisha kwenye akaunti yake ya Instagram, Chameleone alimshukuru mfanyabiashara huyo anayeishi Marekani kwa kukatiza likizo yake ili kuandamana naye hadi Marekani.

Chameleone aliahidi mashabiki zake pamoja na familia yake kwamba atarejea salama kutoka Marekani huku akilalamika kwamba hii ndiyo mara ya kwanza anakosa kutumbuiza jukwaani msimu wa Krismasi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *