Waziri wa Nishati na Petroli Opiyo Wandayi leo Alhamisi amezindua ujenzi wa kituo kidogo cha kusambaza umeme katika eneo la Malaba utakaogharimu shilingi milioni 530.
Wandayi aliyezungumza katika kituo cha kitaifa cha vijana cha Echakara, kaunti ndogo ya Teso kaskazini, alisema ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika, changamoto za kupotea kwa umeme mara kwa mara zitashughulikiwa.
Waziri alikiri kwamba kaunti ya Busia haijaunganishwa kikamilifu na umeme na akajitolea kuhakikisha Kaunti hiyo ina umeme sawa na maeneo mengine nchini.
Matamshi yake yaliungwa mkono na Gavana wa Busia, Paul Otuoma na mbunge wa Teso kaskazini Oku Kaunya ambao walielezea wasiwasi wao kutokana na kukatizwa kwa umeme mara kwa mara katika kaunti hiyo hali inayotatiza shughuli za maendeleo