Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin atazuru Kenya Jumatatu na kufanya kikao na mwenzake kutoka Kenya Aden Duale katika makao makuu ya Ulinzi.
Wawili hao wanatarajiwa kusaini mwafaka wa ushirikiano kati ya Kenya na Marekani na baadaye kuwahutubia wanahabari.
Austin ni mwanajeshi mstaafu wa mamlaka ya nyota nne na anahudumu kama Waziri wa 28 wa Ulinzi nchini Marekani.