Waziri wa Kilimo Dkt Andrew Karanja amewataka wakulima kukumbatia ufugaji ngombe wa maziwa kama njia kuhakikisha uafikiaji haraka kwa mfumo wa kiuchumi wa serikali wa Bottom UP.
Dkt Karanja aliyasema haya alipozuru shamba la ufugaji mafahali la shirika la ustawishaji kilimo ADC, mjini kitale kaunti ya Tranz Nzoia .
Waziri alipongeza juhudi za ADC katika kuimarisha ufungaji wa ngombe nchini ikiwemo matumizi ya mbinu za kisasa za kukusanya shahawa na uzalishaji wa mifugo, ambazo aliongeza kuwa sitawakikishia wakulima wanapata aina bora ya ng’ombe wa maziwa kwa gharama nafuu.